Monday, March 19, 2012

AJIRA KWA POLISI

Serikali yashauriwa
kuongeza askari

SERIKALI imetakiwa kuongeza ajira kwa jeshi la polisi nchini, ili wasaidie kudhibiti matukio ya uhalifu yanayozidi kuongezeka

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msufini kata ya Chamanzi Manispaa ya Temeke Bw.Mharami Mlawa, alisema hali ya usalama si nzuri katika mtaa wao kwa kuwa siku chache zilizopita majambazi walivamia na kuiba vitu mbalimbali.

Alisema kumekuwa na matukio ya ujambazi katika eneo hilo, licha ya wao kushirikiana na viongozi wengine kuhimiza ulinzi shirikishi. Alisema wananchi wamepata elimu hiyo lakini kama kungekuwepo na magari ya doria na askari wa kutosha uhalifu ungepungua

"Siku chache zilizopita wezi walivamia kwa mfanyabiashara mmoja na kupora fedha, lakini polisi waliofika kutoa msaada ni wa kituo cha Mbagala wakati Chamanzi nako kuna kituo na silaha.

Alisema tatizo lingine linalochangia uhalifu ni kukatika kwa umeme  katika baadhi ya vitongoji vya kata hiyo ambapo wahalifu wanatumia fursa hilo kufanya uhalifu.

No comments:

Post a Comment