Anayedaiwa kufanya mauaji Ufaransa auawa
PARIS,Ufaransa
KAZI ya polisi kuzingira nyumba alimokuwaakiishi mtuhumiwa wamauaji katika mji wa Toulouse nchini Ufaransa imemalizika kwa mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuua watu saba kuuawa,
Tarifa hiyo ilithibitishwa jana na , vyanzo vya habari nchini humo ingwa kwamba hakuna uthibitisho rasmi kutoka vyombo vya usalama na serikali.
Polisi aliingia gorofa ambapo,Bw. Merah Mohammed alikuwa amejichimbia baada ya kuzingira jengo hilo kwamuda wa zaidi ya siku moja.
Vyanzo vya habari vya polisi vililiambia Shirika laHabari la Ufaransa AFP kwamba maofisa watatu walijeruhiwa,na mmoja wao vibaya katika shambulizi hilo.
Bw.Merah, (23), alikuwa anatuhumiwa kwa mauaji ya watu saba katika mashambulizi matatu tofauti.
Mapema Waziri wa Mambo ya Ndani,Bw. Claude Gueant alisema Bw.Merah alitaka kufa "na silaha mkononi" na kulikuwa hakuna mawasiliano pamoja naye mara moja.
Kabla ya shambulizi ulifanyika, Bw Gueant alisema ni wazi kama Bw.Merah bado yu hai.
Hata hivyo, polisi alikutana na upinzani wakati walipoanza kushambuliwa muda mfupi baada ya kuvamia jengo hilo(BBC).
Thursday, March 22, 2012
Breaking News, Rais Mali apinduliwa
Wanajeshi Mali wachukua nchi
BAMAKO,Mali
WANAJESHI walioasi nchini Mali wametangaza kwamba wamechukua udhibiti wa nchi ikiwa ni saa kadha baada ya kuvamia kasri ya rais.
Habari kutoka nchini humo zinaeleza kwamba wanajeshi hao walitoa tangazo hilo mapema jana huku wakipiga marufuku mtu yoyote kutoka nje nchi nzima na kwamba katiba haitatumika kwa sasa.
Kwa mujibu wataarifa hizo mapema juzi, wanajeshi hao walifyatuliana risasi na wanajeshi watiifu kwa serikali,wakisema kuwa serikali haijawapa silaha za kutosha kukabiliana na waasi wa jamii ya Tuareg.
Tayari walikuwa wamechukua udhibiti wa kituo cha taifa cha redio na televisheni na kusitisha matangazo.
Baada ya saa kadhaa ya kuonesha picha za nyimbo za wanamuziki wa Mali, kundi la wanajeshi likaonekana kwenye televisheni mapema jana wakitambulishwa kama "Kamati itakayorudisha Demokrasia na kutuliza hali katika nchi".
Msemaji wa waasi hao, aliyetajwa kwa jina la Luteni Amadou Konare, alisema sasa wamemaliza "utawala usio thabiti" wa Rais Amadou Toumani Toure
"Sisi walinzi wa Jamhuri na watu wake, tumelazimika kuchukuwa madaraka kutoka utawala ulioshindwa wa Amadou Toumani Toure na tutayakabidhi madaraka hayo kwa serikali itakayochaguliwa kidemokrasia." alisema Luteni Konare.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wanajeshi hao sasa wameunda chombo walichokiita Kamati ya Kitaifa ya Kurudisha Utawala wa Kidemokrasia baada ya kuwatia nguvuni mawaziri kadhaa wa serikali ya Rais Toure.
Mwanajeshi mmoja aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kwamba, miongoni mwa walio chini ya ulinzi ni Waziri wa Mambo ya Nje, Bw.Soumeylou Boubeye Maiga, na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw.Kafouhouna Kone.
Chanzo huru cha habari kilisema kwamba Rais Toure mwenyewe, ambaye mwanzoni walikuwa amezingirwa ndani ya kasri yake, alifanikiwa kuondoka eneo hilo salama na bado haijulikani alipo rais huyo, ambaye mwenyewe aliingia madarakani kwa mara ya kwanza kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1991.
Mapema nyakati za alfajiri kwa saa za Afrika ya Magharibi, milio ya silaha nzito na bunduki ilisikikana karibu na kasri hiyo na katika mji mkuu, Bamako, lakini mapambano hayo hayakuchukuwa muda mrefu wala hakujapatikana ripoti za maafa yake hadi sasa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,(UN) Bw. Ban Ki-moon, ametaka kuwepo kwa hali ya utulivu na mazungumzo ya kutatua tafauti zilizopo kidemokrasia.
Ufaransa imewataka raia wa Mali kuheshimu utawala wa kikatiba na imelaani aina yoyote ya vurugu. Hata hivyo, haikusema ikiwa haiutambui utawala mpya wa kijeshi, badala yake mkoloni huyo wa zamani ametaka uitishwe uchaguzi "haraka iwezekanavyo."
Hivi punde, Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imepinga hatua hiyo ya wanajeshi kuchukuwa madaraka kwa nguvu.
"ECOWAS inalaani matendo haya yasiyo maana ya wanajeshi walioasi na inaonya kuwa haitavumilia kwa namna yoyote ile matumizi ya nguvu kama njia ya kutatua matatizo". ilieleza Jumuiya hiyo katika taarifa yake iliyotolewa mjini Lagos, Nigeria.(Reuters/AFP).

Monday, March 19, 2012
AJIRA KWA POLISI
Serikali yashauriwa
kuongeza askari
SERIKALI imetakiwa kuongeza ajira kwa jeshi la polisi nchini, ili wasaidie kudhibiti matukio ya uhalifu yanayozidi kuongezeka
Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msufini kata ya Chamanzi Manispaa ya Temeke Bw.Mharami Mlawa, alisema hali ya usalama si nzuri katika mtaa wao kwa kuwa siku chache zilizopita majambazi walivamia na kuiba vitu mbalimbali.
Alisema kumekuwa na matukio ya ujambazi katika eneo hilo, licha ya wao kushirikiana na viongozi wengine kuhimiza ulinzi shirikishi. Alisema wananchi wamepata elimu hiyo lakini kama kungekuwepo na magari ya doria na askari wa kutosha uhalifu ungepungua
"Siku chache zilizopita wezi walivamia kwa mfanyabiashara mmoja na kupora fedha, lakini polisi waliofika kutoa msaada ni wa kituo cha Mbagala wakati Chamanzi nako kuna kituo na silaha.
Alisema tatizo lingine linalochangia uhalifu ni kukatika kwa umeme katika baadhi ya vitongoji vya kata hiyo ambapo wahalifu wanatumia fursa hilo kufanya uhalifu.

Berbatov
Berbatov kuitema Man Utd
LONDON
WAKALA wa mchezaji nyota wa Manchester United,Mbulgaria, Dimitar Berbatov,Emil Danchev,amesema kwamba mteja wake ataondoka katika klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu ili akacheze nchi yoyote Ulaya.
Wakala huyo alisema ameshakutana na kocha wa mchezaji huyo Alex Ferguson kwazaidi ya mara tatau na ameshakubali kwamba anajaribunkujenga kikosi kipya,kubadili mfumo wa uchezaji na kuongeza aina ya kasi.
"Nimekutana mara tatau na kocha wa Manchester United manager, Alex Ferguson.Tumekubaliana kwamba anajaribu kujenga timu mpya,kubadili mfumo wauchezaji na kuongeza kasi zaidi," Danchev alikiambia kituo cha televisheni cha Bulgarian Canal 3 kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP..
"Kikosi cha Manchester United kijacho hakitamuhussha Berbatov," aliongeza.
Danchev alisema kwamba mshambuliaji wake huyo mwenye umri wa miaka 31 ana mpango wa kuondoka kabisa England na kwenda kujiunga na timu nyingine kubwa Ulaya lakini akasema kwamba hakuna hada ya usajili iliyofikiwa.
Alisema kuwa Manchester United hawatakataa hatua yoyote ya Berbatov kutaka kuhama labda waamuae kumuongezea mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.
Berbatov alijiunga na Manchester United mwaka 2008 akitokea katika timu ya Tottenham Hotspur,lakini siku za hivi karibuni amelipoteza soka lake hali ambayo imezua tetesi kwamba huenda akaondoka.

whitney
Mapya yaibuliwa kuhusu Whitney,yadaiwaailkuwa ni msagaji
NEW YORK,Marekani
IKIWA ni takribani wiki kadhaa tangu mwanamuziki nguli Whitney Houston,afariki, habari nyingine za kushangaza zimeibuka zikidai kuwa mwanama huyo alikuwa ni msagaji.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star la nchini Uingereza, Whitney Houston,alikuwa ni msagaji kwa siri,mlevi wa dawa za kulevya na pombe vitu ambavyo vilisababisha kifo chake.
Hata hivyo tetesi zilikuwa nimeshasambaa kwa takribani miaka 30 kwamba muimbaji huyo alikuwa na mahusiano ya siri na msaidizi wake wa zamani,lakini kwa sasa marafiki zake wameamua kuweka wazi ujinsia wake baada ya mwanamama huyo kufariki.
Mmoja wa wanaharakati wa kutetea haki za mashoga, Peter Tatchell,alisema kwamba kuolewa kwake na Bobby Brown ilikuwa ni zuga tu.
‘Ni muhimu kueleza ukweli kuhusu sula hili la maisha yake,"aliliambia gazeti la Daily Star.
‘Whitney alikuwa mwenye furaha wakati alipokuwa alipokuwa aking'ara miaka ya 1980,wakati akiwa na mahusiano na rafiki yake wa kike.
‘Walikuwa wakipendana sana, Labda kutokuwa na uwezo wa kukubali kueleza ukweli kuhusu jinsia yake ndicho kilisababaisha atumbukie kwenye matumizi ya dawa za kulevya,"aliongeza mwanaharakati huyo.
Aliongeza kuwa baada ya kutumbukia katika ndoa na Bobby Brown mambo ndipo yaka muendea vibaya na hivyo akanza kuporomoka siku hadi siku.

Willbroad Mathias
Lindsay Lohan ajiweka kifungo cha nyumbani
NEW YORK,Marekani
MUIMBAJI na muigizaji nyota nchini Marekani, Lindsay Lohan,ameamua kkujiweka kwenye kifungo cha nyumbani ili kujiepusha hasije kuingia katatani kabla ya kumaliza muda wake wa kuwa chini ya ungalizi.
.
Mtandao wa MTZ uliliripoti juzi kuwa nyota huyo wa kibao cha Mean Girls,amemaua kutoondoka nyumbani kwake kwa muda wa wiki mbili zijazo,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la mahakama la kuitumikia jamii.
Mtandao huo ulieleza kwamba umauzi huo ameufikia baada ya Lohan kushutumiwa kumgonga meneja wa klabu ya usiku wakati akiondoka katika klabu hiyo ya Sayers iliyopo eneo la Hollywood.
Huku akiwa anakana shutuma hizo Lohan,anasema kuwa hataki tena kujiingiza kwenye mikasa wakati akiwa ukingoni kumaliza adhabu hiyo ambayo inatarajiwa kumalizika wiki mbili zijazo.

Subscribe to:
Posts (Atom)